Na Francisca Emmanuel.
SHAHIDI wa kwanza katika kesi ya ubakaji inayomkabili mume wa mwimbaji wa muziki wa injili, Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha (32) ameieleza mahakama jinsi alivyobakwa akiwa kwenye gari na nyumbani kwao.
Shahidi huyo mwenye umri wa miaka 17 (jina limehifadhiwa) ambaye pia ni shemeji wa Mbasha, alidai mbele ya Hakimu Wilberforce Luhwago kuwa Mei 23 mwaka huu, Mbasha alimbaka kwa mara ya kwanza wakati mkewe Flora akiwa hayupo.
Alidai siku hiyo, Flora na mumewe walitoka kwenda kufuatilia CD za video zao za nyimbo huku mtoto wao (jina tunalo) akiwa shuleni.
Alidai alishangaa kuona ghafla Mbasha alirudi nyumbani peke yake na kumlazimisha kufanya mapenzi kisha alimtukana na kumtishia kumdhuru endapo atatoa siri.
Akiongozwa na Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga, shahidi huyo aliendelea kudai kwamba Mei 25 mwaka huu, siku ya Jumapili walikwenda kanisani na waliporudi Mbasha alilalamika kuwa ana njaa hivyo alimpa fedha kununua chipsi.
Alidai baada ya kula, Mbasha alimwambia waondoke nyumbani kwenda kumtafuta Flora ambaye hakuwepo nyumbani siku hiyo.SOMA ZAIDI>>

0 comments:
Post a Comment