Unyanyapaa dhidi ya wanawake ni jinamizi kubwa India
Polisi nchini India wanasema
kuwa msichana mmoja ambaye alijaribu kumtetea babake kwenye baraza moja
la kijiji amepatikana akiwa amekufa.
Msichana huyo mwenye umri wa miaka 15 na babake
waliitwa na wazee wa kijiji katika eneo la Bengal Magharibi kutatua
mzozo kuhusu tingatinga.
Inaripotiwa kuwa msichana huyo alipinga ambavyo babake alitendewa alipodhulumiwa na kisha kutoweka
Palisi wanasema kuwa huenda msichana huyo
alibakwa kabla ya kuuawa kwani mwili wake ulipatikana ukiwa uchi.
Inaarifiwa msichana huyo alikejeliwa na wanakijiji kwenye baraza hilo
kwa kuteta ambavyo babake alidhulumiwa.
Familia ya msichana huyo inasema kuwa
alilazimishwa kutema mate ardhini na kuyaramba mate hayo, kitendo
kinachoonekana kuwa cha unyama sana.
Mahakama zisizo rasmi nchini India hutoa adhabu dhidi ya wanakijiji wanaoonekana kuvunja sheria za kijiji kile.
Vitendo vya dhuluma dhidi ya wanawake nchini
India vimeanza kumulikwa tangu ubakaji wa mwanafunzi mmoja mwaka 2012
kwenye basi la abiria.
Serikali ilidhibiti sheria za ubakaji mwaka jana
baada ya maandamano makubwa kufuatia shambulizi hilo lakini unyanyapa
dhidi ya wanawake bado ni janamizi
0 comments:
Post a Comment