Wednesday, September 17, 2014

Matukio ya mauaji ya watu wasio na hatia, yameendelea kuuandama Mkoa wa Geita, kufuatia watu watatu kuuawa kwa kukatwa mapanga na kuchomwa mkukihuku mmoja akijeruhiwa baada ya mtu mmoja anayesadikiwa ni mgonjwa wa akili kutekeleza unyama wake. Tukio hilo lililotokea jana asubuhi katika kijiji cha Nyamilyango wilayani Geita, na aliyejeruhiwa na kulazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Geita ni Mathayo Sindamsanga, na hali yake imeelezwa ni mbaya. Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk. Adam Sijaona, alithitibisha kupokea miili mitatu iliyohifadhiwa hospitalini hapo pamoja na majeruhi mmoja.
Dk. Sijaona aliwataja waliouawa kuwa ni Pindo Makono, Ndakazi Bertha Masabile na Jacob Bukulu, ambao ni wakazi wa kijiji hicho.
Hata hivyo, mtu huyo aliyesababisha mauaji hayo, alikamatwa na wananchi wenye hasira na kisha kumfikisha kituo cha polisi.
Dk. Sijaona alisema marehemu hao walifariki dunia kutokana na kuvuja damu nyingi mwilini kufuatia muuaji kutumia panga na kuwacharanga na kisha mkuki kuwatoboa miili.

0 comments:

Post a Comment