Mwalimu Galus Focus Nguruwe akiwa amefungwa mnyororo
Ndugu wa mtu anayedaiwa kuwa ni mlemavu wa akili, Galus Focus Nguruwe (35) ambaye ni mwalimu wa sekondari moja mjini Morogoro, wamelituhumu Kanisa la House of Prayer Shield of Faith Christian Fellowship lililopo Boko Magengeni jijini Dar kuwa wamemfunga mnyororo ndugu yao huyo kwa miezi nane mfululizo.
Kwa mujibu wa dada wa Galus, Piencia Focus, ndugu yao huyo alichukuliwa na mke wa mtoto wa dada yao waliyemtaja kwa jina la Doreen kutoka Songea mkoani Ruvuma Januari, mwaka huu bila kuwataarifu ndugu, jambo lililowafanya wamfuatilie na kugundua alipelekwa kwenye kanisa hilo kwa madai ya kufanyiwa maombi.
Dada huyo alisema kuwa aliamua kumtafuta ndugu yake hasa baada ya kupata taarifa kuwa aliko amekuwa akishinda huku amefungwa mnyororo mguuni, hali inayomfanya ajisaidie na kula papohapo.
“Japokuwa alikuwa na matatizo ya akili tangu zamani, lakini alikuwa akitumia dawa zake na alipata nafuu na kufanya kazi yake ya ualimu kwani alikuwa akifundisha shule moja ya sekondari Morogoro,”
alisema Piencia Focus.SOMA ZAIDI>>
0 comments:
Post a Comment