Hii picha ni mtoto Mary Rappyson Ishabakaki mwenye umri wa miaka 4 aliyepotea July 15, 2014. Picha hii haiusiani na habari hapo chini.
Mwanamke mmoja mkazi wa Mchikichini, Mbagala jijini Dar es Salaam, Tatu Nyambwela (30) anashikiliwa na polisi baada ya kutuhumiwa kumuiba mtoto mchanga wa miezi mitatu.Polisi pia inachunguza mtoto wake mwingine wa miaka sita anayeishi naye baada ya kudaiwa kuwa alimpata kwa njia ya udanganyifuTaarifa kutoka eneo hilo zinasema mwanamke huyo alikamatwa wiki iliyopita na kufikishwa katika Kituo cha Polisi Mbagala Maturubai, baada ya majirani kumtilia shaka.Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa mtaa huo, Said Pazi, alisema alipata taarifa hizo kupitia kwa majirani wanaoishi eneo hilo, ambapo baada ya kujiridhisha aliamua kutoa taarifa polisi.
MTOTO AGUNDULIKA
Akielelezea tukio hilo, alisema walikwenda nyumbani kwa mwanamke huyo akiwa pamoja na polisi wawili kwa ajili ya kubaini ukweli wa jambo hilo.
Alisema, walipofika katika nyumba anayoishi mwanamke huyo, walimkuta akiwa amekaa pamoja na mumewe aliyetajwa kwa jina la Adinan Mkanilo (45), na mama mkwe wake Asha Limbanga (80) wakizungumza.

0 comments:
Post a Comment