
YALE
madai kuwa sexy lady wa Bongo Fleva aliyeibukia kwenye Shindano la
Kutafuta Vipaji la Epiq Bongo Star Search 2012, Meninah Abdulkareem ya
kutaka kuolewa na staa wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond
Platnumz’ yamemtoa machozi mwanadada huyo.Sexy lady wa Bongo Fleva
aliyeibukia kwenye Shindano la Kutafuta Vipaji la Epiq Bongo Star Search
2012, Meninah Abdulkareem. Hivi karibuni Meninah na Diamond walizua na
bado wanaendelea kuzua mjadala kila kukicha ambapo taarifa juu ya wawili
hao kutaka kufunga ndoa ya chinichini zinaendelea kusambaa kwa fujo
ambapo mwanadada huyo amelonga na Amani kwa dakika kumi.
Kikizungumza
kwa kujiamini, chanzo makini ambacho kiliomba hifadhi ya jina kilidai
kwamba hakuna ndoa tena kati ya Diamond na Beautiful Onyinye, Wema Isaac
Sepetu na kwamba ndoa inayopangwa kwa sasa ni ya Meninah na Diamond.
Chanzo hicho kilinyetisha kwamba
wawili hao walikutana kwa mara ya kwanza kwenye sherehe za utoaji wa
Tuzo za Kili mwaka 2014 na tangu hapo wamekuwa na ukaribu unaodaiwa
unataka kuzaa ndoa.
WEMA AMWINDA
Ilisemekana kwamba baada ya Wema
kuzinyaka habari hizo kuwa anataka kunyakuliwa ‘beibi’ wake mbaya zaidi
wanataka kufunga ndoa, malkia huyo mkubwa wa sinema Bongo aligeuka mbogo
na kuanza kuweka mikakati ya kumteketeza Meninah asiweze kufunga ndoa
na Diamond.
0 comments:
Post a Comment