Cherise Makubale wa Zambia ndiye alikuwa mshindi wa kwanza wa Big Brother
Uzinduzi wa makala mapya ya
kipindi maarufu cha Big Brother nchini Afrika Kusini umeahirishwa baada
ya moto mkubwa kuteketeza studio za kipindi hicho mjini Johannesburg.
Kipindi hicho kilistahili kuanza Jumapili hii
lakini waandaaji wa wa kipindi chenyewe wameamua kuahirisha uzinduzi
huku wakitafuta sehemu nyingine ya kupeperushia kipindi hicho.
Hakuna aliyejeruhiwa kwenye mkasa huo wa moto na kilichousababisha bado hakijajulikana kwani uchunguzi untarajiwa kufanywa.
Washiriki katika kipindi hicho kutoka nchi 14 Afrika watakuwa wanashiriki katika makala ya 9 ya kipindi hicho.
Kipindi chenyewe kinatarajiwa kupeperushwa kwa siku 99 kabla ya mshindi kutangazwa.
Mshindi wa mwaka huu anatarajiwa kupokea kitita cha dola 300,000 kima sawa na kile kilichotolewa kwa mshindi mwaka 2013.
Waandalizi wa kipindi hicho Endemol na M-Net
walisema kuwa juhudi za kupata sehemu mbadala ya kuendeshea kipindi
hicho itakuwa kazi ngumu kutokana na ukosefu wa teknolojia inayohitajika
kuendeshea kipindi hicho kwani haipatikani kwa urahisi.
''Kila juhudi italenga kupata ufumbuzi haraka
iwezekanavyo kuhakikisha kuwa kipindi hicho ambacho hutazamwa na watu
wengi zaidi Afrika kitaendelea.''waliongeza kusema waandalizi.
Waandalizi pia walisema kuwa washiriki kutoka
Ghana walipata tatizo la viza na hivyo wakaamua kuchua raia wa Ghana
wanaoishi nchini Afrika Kusini kwenyewe.
Pia washiriki wapya walitarajiwa kutoka Rwanda
na Sierra Leone kwa mara ya kwanza lakini kutokana na changamoto za hapa
na pale hawataweza kushiriki.
Kipindi cha Big Brother ni kipindi maarufu sana
Afrika kutokana na kupendwa sana kwake, na kilianza kupeperushwa mwaka
2003. Washiriki kutoka Tanzania, Angola, Nigeria, Namibia, Zimbabwe na
Afrika Kusini wamewahi kushinda katika makala ya awali.
Mnamo mwaka 2010, kipindi hicho kiligonga vyombo
vya habari baada ya mshiriki mmoja kutimuliwa kutoka katika nyumba hiyo
baada ya kumpiga makonde mshindani mwanamke
0 comments:
Post a Comment