Mwandishi Mmarekani Steven Sotloff aliyeuawa kwa kunyongwa na wapiganaji wa kiisilamu
Rais wa Marekani Barack Obama amesema kuwa Marekani haitatishwa na
mauaji wa mwandishi mwingine wa habari Mmarekani na kundi la Islamic
state
Akiongea na waandishi wa habari nchini Astonia Rais obama amesema
kuwa mauaji hayo yanaichochea Marekani kukabiliana ziani na magaidi
Mapema Marekani ilisema kuwa kanda ya video inayoonyesha kuchinjwa kwa mwandishi huyo Steven Sotloff ni ya ukweli
Video hiyo iliyotolewa na kundi la wanamgambo wa
Islamic State inamuonyesha mwanamme aliyejifunika uso wake na kisu
mkononi akisimama juu ya Sotlof.
Nchini uingereza waziri mkuu David Cameron
ameongoza mkutano wa kamati ya dharura ya serikali kujalidili jinsi
itakavyojibu tishio la kutaka kumuua mateka raia wa uingereza.
Kwenye video hiyo mwanamgambo aliyejifunika uso
na anayezungumza kiingereza anayaonya mataifa ya kigeni na kuyataka
kusitisha harakati zao dhidi ya kundi la Islamic State.
Sotlof ni mwandishi wa pili wa Mmarekani kuuawa
kwa kukatwa kichwa ndani ya mwezi mmoja baada ya mwandishi mwingine
James Foly kuuawa kwa kukatwa kichwa mwezi uliopota na wanamgambo wa
ISIS.
0 comments:
Post a Comment