SERIKALI kupitia wizara ya habari na utamaduni na michezo imeombwa kushirikiana na taasisi binafsi kwa kukutanisha makabila mbalimbali ili kuondoa chuki binafsi baina ya kabila moja na makabila mengine.
Tamasha hilo la utamaduni ambalo hufanyika kwa mwaka mara moja limekutanisha makabila mbalimbali ambapo makabila hayo waliimba nyimbo zao za asili zenye jumbe mbalimbali za kuelimisha jamii
Vilevile Tamasha hilo lilifanyika Kijiji cha Haydom wilaya ya Mbulu Mkoa wa Manyara ambapo makabila matano yalikutana kwa lengo la kuonesha asili zao ambayo ni Wahdhabe, Wadatoga Wairaq,Wamangati pamoja na kikundi cha sangarasasi kutoka Dodoma ,ambapo walijenga nyumba zao za asili katika kambi hiyo huku wakijipikia vyakula vyao vya asili ambacho kilikuwa kivutio kikubwa kwa wageni waliofika katika tamasha hilo.
Pia makabila hayo walicheza mbalumbali kama kurusha mishale ,mchezo wakuchapana na fimbo pamoja na mashindano ya ngoma zao za asili ambapo kila tamaduni walionesha umahiri wake kwa makabila mengine.
Moja ya ngoma zilizotumbuiza ni ngoma ya Sang’arasasi kutoka Dodoma ambapo mwenyekiti wa ngoma hiyo ni bwana Samweli Mandoo ambapo alisema kuwa kupitia ngoma hiyo ni njia mojawapo ya ajira tegemezi kwani wao hufanya shughuli za ujasiriamali kupitia vikundi vyao na kuweza kujikwamua kimaisha .
Aliendelea kusema kuwa vijana wanaomaliza elimu zao na wale ambao hawajamaliza wanatakiwa kujiunga na vikundi mbalimbali vya utamaduni ili kuweza kudumisha asili yao ya kuzaliwa pamoja na kuweza kuwarithisha asili hiyo watoto wao kwa lengo la kuifanya isipotee.
“tumekuwa tukifanya shughuli hizi hizi kwa kutengeneza vitu mbalimbali kama ngoma ,vinanda mikeka jambo ambalo limekuwa ninjia nzuri kwetu kujitengenezea ajira na kuacha utegemezi”alisema bwana Mandoo
Mbwana Mandoo aliwataka vijana Kote nchini kutosubiri ajira kutoka serikalini bali wanaweza wakajiunga na vikundi mbalimbali vya utamaduni ili kuondoa dhana ya kuajiriwa na kuweza kujiajiri wenyewe na kupunguza wimbi la vijana wa mitaani.
Kwa upande wake Mratibu wa Tamasha hilo la Utamaduni Bwana Paulo Amani alisema kuwa Mtu anayekataa tamaduni yake ni mfu kwani utanaduni ndiyo utambulisho wa mtu na asili yake katika jamii nyingine,
Bwana Paulo alieleza kuwa Lengo la Tamasha hilo ni kuleta jamii za karibu zinazozunguka kijiji cha Haydom kuja kwa pamoja na kusherehekea utamaduni wao ambapo walikaa katika kambi hilo kwa muda wa siku tatu.
“Watanzania tumerudi nyuma katika kudumisha tamaduni zetu tumekuwa tukiiga mitindo ya watu kutoka nje jambo ambalo ni kinyume cha maadili na kupoteza asili ya tamaduni zetu”alisema bwana Paulo
Pia aliendelea kusema kuwa Watanzania wanatakiwa kuenzi utamaduni wao na kuacha kuiga tamaduni za nje kwani utamaduni wetu ni utalii tosha ambalo linaweza kuongeza pato la taifa.
Hata hivyo aliitaka serikali kushirikiana na taasisi binafsi ili kuhakikisha suala la utamaduni linaheshimiwa na kuthaminiwa ikiwa ni pamoja na kuweka watu sahihi katika idara husika wanaoweza kuendesha sekata hiyo kwa umakini.
0 comments:
Post a Comment