Sam Mapenzi, Joniko Flower na Hashim Donode wakiwapa raha mashabiki wa Skylight Band kwenye Nyama Choma Festival iliyofanyika miwshoni mwa juma katika viwanja vya michezo vya chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Mashabiki wakiwa wameshona kwenye viwanja vya michezo vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika Nyama Choma Festival huku Skylight Band wakitoa burudani ya aina yake.
Aneth Kushaba AK47 akitoa burudani sambamba na Digna Mbepera kwa mashabiki wa muziki wa Live Band kwenye tamasha la Nyama Choma lililofanyika mwishoni mwa juma katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam UDSM.
Pale Aneth Kushaba AK47 (hayupo pichani) anapogusa mashabiki na uimbaji wake.
Ni hisia tu hakuna kingine....Skylight Band ni balaa.!
Aneth Kushaba AK47 akishambulia jukwaa kwenye tamasha la Nyama Choma lililofanyika mwishoni mwa juma kwenye viwanja vya michezo vya Chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Nyomi la kufa mtu... hapa chezea Skylight Band ndio habari ya mujini kwa sasa.
Mashabiki wa Skylight Band wakijiachia kwa raha zao.
Mmoja wa mashabiki akiwa ameshika kiuno kuhamaki kwa kile anachokiona jukwaani kutoka kwa Skylight Band kwenye tamasha la Nyama Choma.
Aneth Kushaba AK47 akiwapa vionjo vya aina yake mashabiki wa Skylight Band kwenye tamasha la Nyama Choma.
Digna Mbepera wa Skylight Band akifanya yake jukwaani kwenye tamasha la Nyama Choma lililofanyika kwenye viwanja vya michezo vya Chuo kikuu cha Dar es Salaam-UDSM mwishoni mwa juma.
Sam Mapenzi akiporomosha mistari kwa mashabiki wa Skylight Band Nyama Choma Festival.
Ni burudani mwanzo mwisho.
Sony Masamba akiwachizisha mashabiki wa Skylight Band Nyama Choma Festival.
Mpiga solo wa Skylight Band Allen Kiso Mzuzu akionyesha mbwembwe zake mbele ya camera yetu.
Wapiga vyombo wa Skylight Band wakiwajibika kuhakikisha mashabiki wanapata kitu roho inapenda.
Mwanamanyoya akirekodi video clip ya mpiga drums wa Skylight Band Idirsa (hayupo pichani) baada ya kukunwa na upigaji wake.
Mashabiki wa Skylight Band wakisebeneka na burudani kutoka kwa Sony Masamba na Joniko Flower (hawapo pichani).
Sony Masamba (kushoto) na Joniko Flower wakishambulia jukwaa huku mpiga gitaa la solo wa Skylight Band Allen Kiso Mzuzu akiwasindikiza wakati wa tamasha la Nyama Choma mwishoni mwa wiki jijini Dar.
Mwanamanyoya akiwatunza Joniko Flower na Sony Masamba kwenye Nyama Choma Festival iliyofanyika mwishoni mwa juma.
Pichani juu na chini ni mamia ya mashabiki wa Live Music wakishuhudia burudani kutoka Skylight Band.
Mary Lucos akitoa burudani kwa wakazi wa Dar waliofurika kwenye tamasha la Nyama Choma huku akipewa sapoti na Digna Mbepera.
Joshua Ndege (kushoto) akishow love na swahiba wake.
Super Model Neema Mbuya aking'ara ndani ya Nyama Choma Festival.
U-Selfie ulihusika na ripota wako Zainul Photo kutoka viwanja vya michezo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Nyama Choma Festival.
Hashim Donode wa Skylight Band akishow love na murembo.
Sam Mapenzi akishow love na mashabiki wake kwenye tamasha la Nyama Choma lililofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar.
Mdau mkubwa wa Skylight Band Alois Ngonyani akipata ukodak na mai wife wake.
Alois Ngonyani na mkewe akishow love na marafiki zake waliokuja kushuhudia burudani ya Skylight Band kwenye tamasha la Nyama Choma liliofanyika mapema wikiendi hii kwenye viwanja vya michezo vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Wadau wakisho love na ukodak.
Rais wa Wanamanyoya na vijana wake wakishow love.
0 comments:
Post a Comment