Kufuatia hali hiyo askari wawili kati ya wanne waliokuwa kituoni hapo walipoteza maisha huku wengine wakijeruhiwa vibaya sehemu mbalimbali za miili yao.
Akiongea na blog hii mganga mkuu wa wilaya ya Bukombe Dkt Honorata Rutatinisibwa amekiri kupokea miili ya askari wawili wa kike na kiume ambao ni WP 7106 PC Uria Mwandiga na askari namba G.2615 Pc Dustani Kimati.
Askari waliojeruhiwa katika tukio hilo kuwa ni pamoja na mwenye namba E.5831 CPL David Ngupama Mwalugelwa aliyejeruhiwa kichwani na usoni na kwamba ameumizwa vibaya sehemu za midomo yake huku meno mawili yaking'oka na Mohamed Hassani Kilomo ambye amejeruhiwa kifuani na mguu wa kulia uliovunjika mfupa kwa kupigwa risasi.
Kwa mjibu wa Dr Honoratha kutokana na hali za majeruhi kuwa mbaya wamewapa rufaa kwenda hospitali ya rufaa ya Bugando kwa matibabu zaidi.
Kamanda wa polisi mkoa wa Geita Joseph Konyo amethibitisha kutokea kwa tukio na kuahidi kutoa taarifa zaidi mara baada ya uchunguzi kukamilika.

Very bad..... hao majambani ni lazima wakamatwe na kuteswa sana.
ReplyDelete