Posted by Williammalecela.com on Tuesday, September 30, 2014
 |
RAIS KIKWETE KUZINDUA BARABARA YA MWENGE –TEGETA. 30/9/2014 Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete anatarajiwa
kuwa mgeni rasmi katika sherehe za ufunguzi wa barabara ya Mwenge
–Tegeta yenye urefu wa kilometa 12.9 katika eneo la Lugalo, jijini Dar
es salaam. Taarifa iliyotolewa leo
jijini Dar es salaa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Muhandisi Musa
Iyombe imeeleza kuwa sherehe za ufunguzi wa barabara hiyo zitafanyika
tarehe 1, Oktoba ,2014 katika eneo la Lugalo njia panda ya Kawe kuanzia
saa nne asubuhi. Taarifa hiyo imeeleza kuwa kukamilika kwa upanuzi
wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 12.9 ni sehemu ya mkakati wa
serikali wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es salaam. MWISHO. |
0 comments:
Post a Comment