Tuesday, September 2, 2014

1Afisa ufundi wa kilimo cha mboga kutoka TAHA Bw. Abdon akiwaelekeza wakulima kuhusu mbinu bora za uoteshaji wa miche ya mboga kwenye trei maalumu katika mahadhimisho ya siku ya wakulima shambani kwa wakulima wa kijiji cha Mferejini-Machame katika  wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro.2Katibu tawala wa Wilaya ya Hai Bi. Zuhura Chikira ambaye alikuwa mgeni rasmi, akisiliza maelezo kutoka kwa mtaalamu wa kilimo cha mboga kutoka TAHA Bw. Giliard Daniel katika mahadhimisho ya siku ya wakulima shambani kwa wakulima wa kijiji cha Mferejini-Machame katika  wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro.
6Mzee Shabani Shoo akizungumza na wakulima (hawapo pichani)kuhusu mbinu alizofundishwa na wataalamu
7Wakulima wakimsikiliza mtaalamu wa masuala ya mbolea na viatilifu kutoka kampuni ya Triachem Bi.Baby Nkassa
wakati akizungumzia suala zima la matumizi fasaha ya mbolea na viatilifu kwenye mazao
10Wakulima wakifatilia maelezo kutoka kwa mtaalamu wa kilimo cha mboga mboga kutoka TAHA Bw.Collins Okiya wakati wa mafunzo hayo
Asasi ya sekta binafsi ya wakulima wa mboga mboga,Matunda, maua, viungo na mbegu zake imehadhimisha siku ya wakulima shambani kwa wakulima wa kijiji cha Mferejini-Machame katika  wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro.
Maadhimisho hayo yamekuwa yakifanyika kila baada ya Mwezi mmoja mpaka miwili ili kutoa fursa kwa wananchi kujifunza mbinu bora za kilimo cha mazao ya ‘horticulture’ ikiwa ni sambamba na kujifunza mbinu fasaha za kilimo biashara.

0 comments:

Post a Comment