
Na baraka Mbolembole, Dar es Salaam,
Salum
Telela alifunga bao pekee kwa kuunganisha krosi ya mshambulizi Didier
Kavumbangu na kuisaidia timu yake kupata ushindi wa bao 1-0 katika
mchezo wa Ngao ya Jamii, mwaka uliopita.. Kelvin Yondan, Nadir Haroub,
Saimon Msuva, ni wachezaji pekee ambao wanaweza kuanza moja kwa moja
katika kikosi cha kwanza cha Mwalimu, Marcio Maximo. Mfungaji wa mwaka
uliopita Telela na mlinzi wa kulia Juma Abdul ambao wote walianza katika
mchezo wa ushindi mwa jana, mmoja wao atasubiri katika benchi ili
kupisha utitiri wa viungo katikati ya uwanja.
Aishi
Manula, Erasto Nyoni, David Mwantika, kaimu nahodha Aggrey Morris,
Himid Mao Mkami, Salum Abubakary, Kipre Tchetche, Kipre Bolou wote hao
walianza katika mchezo wa kichapo mwaka jana na wanataraji kuanza katika
mchezo wa leo ambao utakuwa watatu mfululizo kwa kikosi chao cha Azam
FC katika Ngao ya Jamii. Mabingwa hao wa ligi kuu Bara msimu uliopita,
wana safu kabambe ya mashambulizi ambayo ilifunga mabao 12 katika
michezo mitano ya Kagame Cup, Mwezi uliopita nchini Rwanda.
Wakati
kocha wa Yanga, Maximo akitaraji kumuanzisha mshambulizi mmoja mbele,
huku akitegemea safu ya kiungo kama muhimili wa timu, Joseph Omog yeye
yupo tofauti , licha ya kumkosa nahodha wake John Bocco, kocha huyo raia
wa Cameroon atakuwa na nafasi nzuri ya kujaribu safu yake ya ‘
washambulizi watatu wa kimataifa’. Tchetche, Mhaiti, Lieonel Saint na
Mrundi, ‘ Kavu’ ambaye alifunga mabao 22 katika misimu miwili ya ligi
kuu Bara akiwa na kikosi cha Yanga. Yanga watapata shinda lakini sehemu
yao ya katikati ya uwan ja inatakiwa kuwa ngumu zaidi ya ilivyokuwa
katika michezo minne iliyopita ya maandalizi ambayo wameshuhudia timu
yao ikifunga mabao matano tu.
AZam
ni lazima watafunga, wanaweza kufunga hata mabao mawili kwa sabu safu
yao ya mashambulizi ina wafungaji wa uhakika. Kama Leonel ataachana na
tabia yake ya kutotoa ushirikiano na kujiona staa zaidi ya wenzake
itaendelea Azam itaanguka na wanaweza kupoteza mchezo. Safu ya ulinzi ya
Yanga ndiyo ile inayotumika katika timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa
Stars, golikipa Deogratius Munish ana nafasi kubwa ya kuanza mchezo huo
lakini nafasi hiyo inaweza kuangukia kwa ‘ mwalimu wa uwanjani’ Juma
Kaseja, nahodha Nadir, Kelvin a Oscar Joshua katika upande wa kushoto
ni nafasi nne ambazo zinapangika kwa urahisi.
Maximo
kama ilivyo kwa Omog naye atakuwa akikuna kichwa, ni mlinzi gani sahihi
wa kulia ambaye anatakiwa kumpanga katika mfumo wake na kufanya vizuri.
Abdul au Telela? Ogog atakuwa akitafakari nafasi hasa ya kumpanga Nyoni
mchezaji ambaye anaingia katika mifumo yote. Nani atamchezesha nafasi
ya ulinzi wa kushoto? Ni Nyoni, Said Mourad au kinda Gadiel Michael
ambaye alifanya vizuri katika michuano ya Kagame?. Makocha wote
wanapasuka vichwa, hiyo ni kutokana na wachezaji wa timu pinzani jinsi
wanavyocheza na u-fit wao walionao sasa.

Maximo
amekuwa akitumia mfumo wa 4-5-1 ambao huwapanga viungo watano, Hasan
Dilunga upande wa kulia, Mbuyu kama kiungo wa kwanza wa ulinzi-namba
6, Andrey Coutinho kama kiungo wa mashambulizi akitokea upande wa
kushoto, Niyonzima kama kiungo ‘ mchezesha timu mkuu’ –namba 8, Msuva
amekuwa akitumika kama mshambulizi wa pili. Kwa nini imekuwa hivyo?
Mbuyu ni mkabaji hasa na mchezaji anayeanzisha pasi nzuri kwa viungo wa
mbele. Dilunga ni mchezaji mwenye nguvu katika miguu na mwili wake , ni
mwepesi hivyom ni rahisi kwake kucheza kama kiungo wa kulia, wakati
mwingine upande wa kushoto, kama ataendelea kupiga pasi zinazofika bila
shaka ni chaguo ambao Maximo hatajutia. Vipi kuhusu nafasi ya Mrisho
Ngassa? Maximo anaweza kumpanga Nassa kama mshambulizi wa pili nyuma ya
GEilson Santos ‘ Jaja’ na ikiwa hivyo itamaanisha Dilunga arudi katika
benchi na Msuva acheze kama kiungo wa kulia. Itafaa zaidi , Ngassa
akicheza, kwa sababu viungo wa Azam ni ‘ wagumu na hawachoki’ mapema.
Himid, Salum, na Bolou itakuwa safu nzuri ya kiungo kwa upande wa kikosi
cha Omog, lakini anaweza kumtumia Nyoni katika eneo hilo ikiwa
atachezesha timu yake katika mfumo wa 4-4-2.
Azam
wana safu nzuri ya ulinzi ambayo kwa kiasi kikubwa ilichangia mafanikio
ya timu hiyo katika ligi kuu Bara msimu uliopita waliporuhusu mabao 15
katika michezo 26. Morris, Mwantika ni chaguo zuri la kwanza katika safu
ya ulinzi wa kati. Jaja atafunga katika mchezo wa leo ikiwa viungo wake
watamiliki mchezo. Shomari Kapombe atakutana na kiungo mwenye maarifa,
Couinho na upande wa kulia wa Azam umekuwa na mchezo usioridhisha sana
kwani upande huo upitika kiurahisi, ili kuziba nafasi ya Yanga kutumia
upande wao wa kushoto Omog ni lazima amuanzishe nje mshambulizi wake
mmoja ili kumpatia nafasi Nyoni katika eneo la kiungo kuwasaidia, Himid,
Salum na Bolou.
Said
Mourad atakuwa na nafasi finyu ya kuanza katika safu ya ulinzi wa kati,
lakini ili kuleta usawa na nguvu zaidi katika ngome, Omog anaweza
kupata faida kubwa akimpanga mchezaji huyo katika eneo la ulinzi wa
kushoto. Ni mechi ngumu lakini inaweza kuwa ya mabao mengi, 3-2, 2-1 au
3-1 ni matokeo ambayo yanaweza kutokea. Ipi timu bora zaidi katika
mchezo wa leo? Yanga? Ubora wao uko wapi?
Azam
ikiimaliza sehemu ya kiungo ya Yanga watashinda, ila watafungwa
wakiruhusu vipaji vya Yanga kutawala katikati ya uwanja. Kavumbagu
atafunga, Jaja atafunga ila ningempanga Telela katika eneo la kiungo la
Yanga ili kuwamudu Azam FC ‘ mwanzo-mwisho’. Ningempanga Nyoni katika
kiungo na Mourad katika safu ya beki tatu ili kupunguza krosi za Yanga.
Yanga ina nafasi ya kushinda kwa mara nyingine….AZam FC ililazwa na
Simba SC kwa mabao 3-2, 2012, wakapoteza mbele ya Yanga kwa bao 1-0,
2013, 2014 itakuwaje, Ngao ya Jamii si bahati yao?
0714 08 43 08
0 comments:
Post a Comment