Wednesday, September 17, 2014

Mwili wa Melasi Lutebula Ndabi ukiwa umetupwa baada ya kuchinjwa.
 Mfanyabiashara aliyefahamika kwa jina la Melasi Lutebula Ndabi ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa  Kamati ya Ulinzi  na Usalama Mtaa wa Muhimbili 2, Kata ya Pemba, Wilaya ya Temeke jijini Dar, ameuawa kwa kuchinjwa na watu  wanaodaiwa kufika kwake kwa ajili ya kukodi shamba la kulima matikiti.Habari zinadai kuwa, marehemu mbali na kuwa mfanyabishara na kiongozi katika eneo hilo, pia alikuwa akijishughulisha kwa kilimo na ufugaji, kazi ambazo amekuwa akizifanya tangu afike  katika eneo  hilo mwaka 2005.

Akizungumza kwa uchungu na Uwazi, mke wa marehemu aitwaye Rehema Shaban (pichani),  alisema siku za nyuma kuna watu watatu walifika nyumbani hapo wakihitaji kukodi shamba kwa ajili ya kulima matikiti.

Watu hao ambao inadaiwa si wakazi wa eneo  hilo na wala hawajulikani walisema wanatokea Kijiji cha Lisu wilayani  Nzega, Mkoa wa  Tabora  walielekezwa  kwa  marehemu huyo. 
Ilielezwa kuwa, kwa mara ya kwanza watu hao walifika  nyumbani kwa marehemu Septemba 5, mwaka huu baada ya mazungumzo ya kina, marehemu aliwaonesha eneo la ekari tatu.SOMA ZAIDI>>


0 comments:

Post a Comment