Akitoa mada juu ya uandishi wa habari za uchunguzi juu ya ukatili wa kijinsia mtoa mada katika warsha hiyo Mwandishi Mkongwe hapa nchini Deo Mushi amewahimiza waandishi wa Habari kuandika na kuibua habari za unyanyasaji wa wanawake na watoto unaofanyika kwa wingi katika maeneo mengi hapa nchini.
Ameeleza waandishi wanatakiwa kuandika habari za uchunguzi zenye ukweli ili kuibua vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto vinavyofanyika majumbani na maeneo mengine katika jamii.
Mushi ameleza kuwa upo ukatili mkubwa unafanyika miongoni mwa jamii katika maeneo mengi hapa nchini na waandishi wa Habari ni wajibu wao kuhakikisha wanaandika unyanyasaji huo na kuibua katika jamii na kuweka wazi ili jamii ielewe na kuacha kufanya vitendo hivyo vya unyanyasaji.
“Kwa kuwa waandishi wa Habari ni muhimili katika jamii na pia ni muhimili wa nne katika nchi ingawa hauna meno ni muhimu sana kusaidia kuibua uovu na manyanyaso yanayofanyika kwenye jamii ”.
Kwa upande wake Mwezeshaji kutoka TAMWA Judica Lusayi akiwasilisha mada inayohusu Chama cha waandishi wa Habari wanawake Tanzani Media Woman Association (TAMWA) naukatili wa kijinsia alieleza kuwa TAMWA ni chama cha waandishi wa Habari ambapo kipo kwa ajili ya kutetea haki za wanawake na watoto katika jamii.
Akitoa mifano alieleza kuwa upo unyanyasaji mkubwa wa kijinsia katika jamii ambapo alitaja baadhi ya unyanyasaji wa kijinsia kuwa upo wa aina mbalimbali,baadhi ya unyanyasaji huo alitaja kuwa ni ndoa za utotoni,ukatili wa starehe,ukatili wa kijamii na kiuchumi.
Unyanyasaji mwingine ulitajwa kuwa ni unyanyasaji wa kisaikolojia,unyanyasaji wa kisiasa,pamoja na unyanyasaji wa kimwili.
Nao waandishi wa habari wa Habari wakichangia katika warsha hiyo walitolea mifano kuwa wanasiasa mkoani kigoma wanatabia ya kuwanyanyasa wanawake wakati wa kampeni za kisiasa wanaoa wanawake ili waweze kupigiwa kura wakati wa uchaguzi na pindi uchaguzi unapomalizika wale wanawake walioolewa huwa wanaachwa huo nao ni unyanyasaji pia vitndo hivyo vinatakiwa vikemewe.
Katika warsha hiyo ya siku tatu jumla ya washiriki 18 kutoka katika mikoa hiyo wa Katavi,Rukwa naKigoma wanahudhuria warsha hiyo,mada zinazojadiliwa ni Ufahamu wa Kkatili wa kijinsia,TAMWA na ukatili wa kijinsia,uchambuzi wa magazeti,wanahabari na ukatili wa kijinsia,changamoto katika Mikoa hiyo pamoja na majukumu katika Mikoa ya Rukwa Kigoma na Katavi.
0 comments:
Post a Comment