Wednesday, October 8, 2014

Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Mahona Salasini (30) mkazi wa Upendo – Chunya aliuawa kwa kuchomwa kisu katika sikio la kulia na katika shavu lake la kulia na mtu aliyefahamika kwa jina la Godfrey Lams (30) mkazi wa mbuyuni – chunya.
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo majira ya saa 03:00 huko katika kitongoji cha Mbuyuni “B”, kata ya Mbuyuni, tarafa ya Songwe, wilaya ya Chunya, mkoa wa Mbeya. 


Chanzo cha mauaji ni wivu wa kimapenzi, kwani inadaiwa kuwa marehemu alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke mmoja aitwaye Melenia Mgata (24) mkazi wa Mbuyuni ambaye awali alikuwa na uhusiano na mtuhumiwa na baadae waliaachana/walitengana.
Mtuhumiwa amekamatwa. Mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi wa kitabibu na kukabidhiwa ndugu kwa mazishi.

0 comments:

Post a Comment