Karibuni sana katika tukio la kihistoria la kukabidhi Rasimu ya Katiba Pendekezwa kwa Rais wa Jamhuri Dr Jakaya Kikwete hapa Dodoma.

Tayari uwanja wa Dodoma umefunguliwa tangu asubuhi saa 12 na kuna idadi kubwa ya Askari kuimarisha ulinzi ndani na nje ya viwanja hivi.

Kuna shamrashamra mbalimbali hapa zikiongozwa na vikundi vya uhamasishaji vya Chama cha Mapinduzi.

Pia kuna Idadi kubwa ya Wageni kutoka mikoa mbalimbali waliokuja kwa usafiri maalum wa mabasi kushuhudia tukio hili la kihistoria.

Pengine DOA kubwa kwa tukio la leo ni ususiaji unaoongozwa na Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA unaoundwa na vyama vikuu vitatu yaani Chadema,CUF na NCCR.

Ni wazi Rais hatafurahishwa kukabidhiwa Rasimu ambayo ni ya Upande mmoja hasa ikizingatiwa serikali ya Zanzibar imegawanyika makundi mawili.Moja la CCM likiunga mkono na la pili la CUF likilaani na kupinga Katiba hii.