Friday, October 17, 2014

Kama ulikuwa unawasiwasi kuwa haitawahi kutokea collabo ya Diamond na msanii mwenzake ambaye alikuwa akitajwa kuwa na tofauti nae Alikiba, sasa unaweza kupunguza mashaka sababu Diamond yupo tayari kuingia booth na mwimbaji huyo wa ‘Mwana’ endapo atatakiwa kufanya hivyo (lakini endapo kama na Alikiba atakuwa tayari kwa ofa hiyo).
Diamond Platnumz amesema yupo tayari kufanya collabo na Alikiba au msanii yeyote atakayehitaji msaada wake. 
“Mimi sina tatizo, inategemea ni project gani inategemea ni muziki gani kwasababu nimeshawasaidia watu wengi nimefanya nao macollabo kwanini mtu anavyokuja nifanye nae collabo yeye nikatae, yaani siwezi kukataa” Diamond ameiambia 255 ya XXL ya Clouds Fm. 

0 comments:

Post a Comment