Wednesday, October 1, 2014

Diamond..Mh! Upepo mbaya unaivumia kapo ya mafahari wawili Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambapo wanadaiwa kufanyiana ‘taimingi’ ya kumwagana, ‘ubuyu’ kamili huu hapa.Staa wa filamu Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’.Kwa mujibu wa mnyetishaji wetu makini, wawili hao wamepotezeana kwa muda mrefu huku kila mmoja akifanya yake lakini kila mmoja anashindwa kujitoa mhanga na kusema hawapo pamoja akihofia kuonekana ndiye tatizo. “Kifupi ni kwamba Wema na Diamond hawapo pamoja kwa kipindi kirefu, yawezekana wanawasiliana lakini si kwa mapenzi labda kwa mambo mengine. Diamond anazuga kama yuko kwenye shoo, hata akirudi Bongo hawana ukaribu na Wema kama ilivyokuwa zamani, anazuga kidogo kisha anaondoka tena.

Mkali wa Bongo Fleva, Diamond Platinum.“Wema naye hivyohivyo, yupo bize na mambo yake, inasemekana yupo na kigogo f’lani hivi Mkongomani ndiye anampa jeuri mjini kama ulivyoona juzikati amemwaga mapesa ukumbini. 
“Inasemekana Mkongomani huyo amemfungulia pia ofisi mpya ya kurekodia filamu pamoja na kumnunulia gari jipya,” kilidai chanzo hicho. 

0 comments:

Post a Comment