Tuesday, October 14, 2014

"Miaka 15 bila Baba wa Taifa,Hayati.Julius Kambarage Nyerere.
Katika nafasi yangu ndani ya Chama na Serikali,Nguvu,Sauti na Matendo yangu nì kutetea wanyonge kama Baba wa Taifa alivyofanya.


Napambana na Wakwepa kodi ili Fedha hizo zitumike Kusomesha Masikini.
Napambana na Mishahara hewa ili Fedha hizo ziwalipe Watanzania waliojitoa kulitumikia Taifa lao.
Napambana na Matumizi mabaya ya Fedha za Umma ili fedha hizo zitumike kujenga Vituo vya Afya n.k kuokoa Vifo vya Mama zetu.
Napambana na Misamaha ovyo ya Kodi ili Watanzania Masikini na Wanyonge wapate Madarasa,barabara n.k
Kitendo cha Kuendelea kuachwa Rushwa,Kuruhusu Ukwepaji kodi na Misamaha ya kodi isiyo na tija ni hatari sana kwa Taifa letu,Kufanya hivyo tunasababisha GEPU kubwa kwa Masikini na aliyenacho "Masikini anaendelea kuwa Masikini na tajiri anaendelea kuwa tajiri".

Kama Taifa tunahitaji kuunganisha nguvu Zetu kupambana na Wakwepa kodi,Rushwa na Watumishi wasio wazalendo kwa Taifa hili.
Tumuenzi Baba wa Taifa kwa Vitendo "Mabadiriko ni VITENDO".
Mungu Ibariki Tanzania."






0 comments:

Post a Comment