Miss
Tanzania namba tatu, Jihan Dimachk. Yameongelewa mengi na kimsingi mpaka
sasa bado ushindi wake unaonekana kuwa na makengeza. Kutokana na hali
hiyo, waandishi wetu walifanya mazungumzo na baadhi ya wadau lakini kati
yao alikuwa mmoja wa washiriki ambaye alichukua nafasi ya tatu, huyu ni
Jihan Dimachk.
Gumzo mtaani
kwa sasa kwenye ulimwengu wa urembo ni ushindi wa mwanadada Sitti Abbas
Mtevu ambaye hivi karibuni aliibuka mshindi katika Shindano la Miss
Tanzania 2014. Tutakumbuka baada ya Sitti kutangazwa mshindi, maneno
yalikuwa mengi, mara alipendelewa, mara alidanganya umri, wengine
wakasema eti ana mtoto.
Kwenye
fainali za mashindano hayo mrembo huyu alichukua Taji la Miss Tanzania
Top Model 2014 na sasa fuatilia exclusive enterview hii iliyofanyika
kati yake na Ijumaa ndani ya Hoteli ya Regency iliyopo Mikocheni, Dar.
Ijumaa: Habari yako Jihan, sisi ni waandishi kutoka Gazeti la Ijumaa.
Jihan: Okey,
nashukuru kuwafahamu, karibuni. Ijumaa: Tuanze na matokeo ya
kinyang’anyiro cha Miss Tanzania mwaka huu, unadhani wewe ulistahili
kuchukua nafasi ya tatu na Sitti Mtemvu kuibuka kidedea?
Jihan:
Siwezi kuongea sana jamani lakini kwa kifupi nilikuwa nikiamini
nitashinda, niseme tu kwamba it was unfair but I can’t explain (haikuwa
sawa ila siwezi kuelezea).
Ijumaa: Kwa nini unasema hivyo? hebu fafanua kauli yako.
Ijumaa: Wapo
wanaosema ulikuwa na kila kigezo cha kuwa Miss Tanzania 2014 lakini
umetoswa kutokana na rangi yako ukihisiwa wewe si Mtanzania,
unaliongeleaje hili?
Jihan: Sipendi kabisa kusikia maneno hayo, mimi ni
Mtanzania, nimezaliwa Mwanza, mama yangu ni Msukuma na baba yangu
Mlebanon. Tangu naingia kwenye shindano hili waandaaji walinihoji,
wakafuatilia hilo na kutambua ni Mtanzania, ingekuwa tofauti sidhani
kama ningeruhusiwa kushiriki.
Ijumaa: Kwa mfano ikitokea Sitti akavuliwa taji kutokana na haya yanayozungumzwa, uko tayari uvishwe wewe?
Jihan:
Siwezi kulijibu swali hilo kwani haijatokea. Endapo itatokea na
waandaaji wakanifuata kuniambia hivyo, hapo ndiyo nitakuwa na la
kuzungumza.
Ijumaa:Unamuongeleaje Sitti Mtemvu? Jihan: Kwa sababu ndiye
aliyevishwa taji, naheshimu ushindi wake, namkubali kuwa ni mrembo na
siwezi kupingana na maamuzi yaliyotolewa.
Ijumaa:
Umechukua nafasi ya tatu ambayo nayo si haba, una mipango gani ya
baadaye?
Jihan: Nina mambo mengi ya kufanya. Nina ndoto za kuwasaidia
wanawake na watoto lakini pia nahisi nina jukumu la kusaidia katika
suala la elimu nchini, nitajipanga kufanikisha hayo. Ijumaa: Kwa nini
elimu?
Jihan:
Nimekuwa nikikutana na watu wengi ambao elimu imekuwa kikwazo kwenye
maisha yao, nikawa nimejiapiza kuhakikisha nawasaidia kadiri
nitakavyoweza. Ijumaa: Asante sana Jihan, tunakutakia mafanikio katika
yale unayopanga kuyafanya.
Jihan: Nashukuru sana.
Source:- Habari Motto Blog
0 comments:
Post a Comment