Alipotangazwa mshindi, Miss Tanzania
2014, Sitti, ambaye ni binti wa mbunge wa jimbo la Temeke jijini Dar es
Salaam, alivikwa taji na mtangulizi wake Happyness Watimanywa, Miss
Tanzania 2013.
Kufikia taji hilo la Miss Tanzania,2014 Bi Sitti ni
mshindi wa mara ya ishirini tangu mashindano hayo yaanze tena nchini
humo mwaka 1994.
Kabla ya taji hilo, Bi Sitti alishinda mataji mawili
likiwemo la Miss Chang'ombe na Miss Temeke yote ya mwaka 2014.
Pia ataiwakilisha Tanzania katika shindano la Miss World 2015.
Warembo 30 waliingia katika kinyang'anyiro cha Miss Tanzania 2014.
Lillian Kamazima alikuwa mshindi wa pili, ambapo Jihhan Dimachk alishika nafasi ya tatu.
Mara baada ya kutwaa taji hilo kumeibuka utata juu ya umri wa Miss Tanzania 2014.
Habari
zimezagaa katika mitandao ya kijamii, ambapo anatuhumiwa kudanganya
umri wake. Kuna taarifa zinasema Bi Sitti alitaja kuwa ana umri wa miaka
18, jambo linalobishaniwa.
Lakini ukweli utajulikana Jumanne
tarehe 21 Oktoba 2014, ambapo waandaji rasmi wa mashindano ya urembo ya
Miss Tanzania, Lino International wameahidi kulitolea ufafanuzi suala
hilo.
0 comments:
Post a Comment