Saturday, October 11, 2014

Mtoto mzuri Bongo Movies, Jacqueline Massawe Wolper.

MTOTO mzuri Bongo Movies, Jacqueline Massawe Wolper, amemtolea uvimu pedeshee maarufu, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mwami Rajabu na kumwambia aache
kumfuatafuata.Mwishoni mwa wiki iliyopita, Mkongo huyo ambaye anajitapa kuwa ameshatembea na baadhi ya mastaa Bongo akiwemo Wolper, alikaririwa katika gazeti hilihili akidai ametembea na Wolper kisha kumwaga na sasa anammendea mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ kwa gharama yoyote. 
Akizungumza na mwanahabari wetu, Wolper alisema anamshangaa mwanaume huyo amekuwa akimfuatafuata na kumzungumzia katika vyombo vya habari wakati hana hadhi ya kuwa na mtu kama yeye.

0 comments:

Post a Comment