Monday, October 27, 2014

Jiko linahitaji kupambwa na usafi baada ya shughuli zako za jikoni unasafisha na kupamba  vizuri kwa mauwa pembeni  safi,hata mgeni akija nyumbani kwako hajiulizi mara mbili kama akikaribishwa chakula.Kuna nyumba nyingine Loh!! unatamani kukimbia ukiambiwa karibu chakula, Ni vizuri kama upo busy sana jaribu kumsimamia mschana wa kazi kuhusu usafi wa jiko na kupanga vyombo vyako sehemu safi.kwa wale wenye Open Kitchen kwa hapa bongo ni vizuri kuwa na  vent- hoods ili kuondoa harufu ya chakula kwenda dining na siting room, sababu ile harufu ya chakula ua inakaa kwenye makochi na mapazia,then utakuta nyumba inanuka shombo ya chakula.
 









Natural ni muhimu ndani ya nyumba ,jaribu  kuwa na mimea kiasi ndani ya nyumba inapendeza pia.Kama mimea natural inakushinda kumaintain basi jaribu hata artificial ila chagua yale yanayo endana na ukweli ..Maua yana pambwa sehemu zote kama,Toilet,Kitchen Room, Dinning,siting room na Bed room na garden yenyewe. weka maua ya kiasi tu ndani ya nyumba maana ya kizidi sana yanakuwa ni kero na uchafu







 

Wengi wetu tumekuwa hatutili maanani chooni sababu tumekuwa na tabia kuwa chooni ni sehemu ya kujisaidia. ,Nachotaka kusema kuwa naomba tupende toilets zetu sababu ndio sehemu kubwa ambayo tunafanyia starehe zetu, Pili  ni sehemu kubwa ya mtu kukupima usafi wako na hustarabu ukifuatiwa na jikoni,ni vizuri kama hutaweza kupamba toilet yako kwa kuweka maua,mirros,Carpet Sets For Toilet And Bathroom  hii itakufanya kuonekana smart,pili kwa wale wenye toilet ya moja kwa moja tujitahidi kufanya kuwa kukavu mda wote hii ni moja ya usafi.











              


0 comments:

Post a Comment