ROMA, Italia
KATIKA
hatua inayooonekana kuwa tofauti na matarajio ya wengi kutokana na msimamo
wake, Kanisa Katoliki hivi sasa linaelekea kwenye hatua za mwisho za kuukubali
ushoga.
Hii inatokana na mkutano wa wakuu wa Kanisa hilo
duniani kutoa wito kwa waumini wake duniani kuwachukulia watu wanaofanya
mapenzi ya jinsia moja kama watu walio na haki na sawa na wengine.
Kauli hii imechukuliwa na watu wengi na hasa wale
wanaoshabikia ushoga duniani kusema kwamba kanisa hilo hivi sasa linaukubali
ushoga.
Aidha, kauli hii inakuja baada ya Maaskofu kuandika ripoti
wakati wa mkutano wa synodi ukiendelea huko Vatican na kusema kuwa wapenzi wa
jinsia moja wana zawadi na viwango vya kutoa kwenye jumuiya za kikristo hii
ikiwa ni ripoti iliyotolewa mapema wiki hii.
Msimamo huo mpya wa Kanisa Katoliki, unaonekana
kuwakera watu wenye msimamo mkali kwenye kanisa hilo na moja ya makundi yenye
kushikilia msimamo mkali ki-kanisa wametupilia mbali ripoti hiyo na kuiita ya
kisaliti.
Zaidi ya maaskofu 200 wa Kanisa Katoliki wanakutana
kwenye mkutano wa synodi tangu mapema mwezi huu, katika mkutano huo ni papa
Francis aliyetoa mwito wa kujadili masuala ya utoaji wa mimba, vidonge vya
uzazi wa mpango, mapenzi ya jinsia moja na talaka.
Papa Francis amewataka viongozi wa juu wa kanisa
hilo kuzingatia zaidi suala la wapenzi wa jinsia moja katika mtazamo chanya
kuliko kuwa kinzani na amefanikiwa kuwateka maaskofu wanaohudhuria mkutano huo
wa sinodi.
Mwaka uliopita katika ripoti aliyoitoa papa Francis
kuhusiana na mwenendo wa Kanisa Katoliki kuwa waumini walio wengi waliliacha
mkono kanisa hilo kutokana na mafunzo yanayohusu ngono na dawa za uzazi wa
mpango.
Papa huyo anazichukulia ndoa hizo za jinsia moja
kama zisizo na utaratibu akiinukuu ripoti ya kanisa katoliki iliyochapishwa
mwaka 1986, wakati Papa Francis alipokua mshauri mkuu wa masuala ya teolojia ya
Kanisa Katoliki wa hayati papa John Paul wa pili.
Moja ya sababu zilizodaiwa kumuondoa kitini
mtangulizi wa Papa Francis, Papa Benedict, ilielezwa kwamba ulikuwa ni mvutano
kati yake na genge la wapenda ushoga ndani ya uongozi wa kanisa hilo huko
Vatican.
Ilielezwa Benedict alikuwa ameshikilia msimamo wake
kwamba kanisa hilo linapaswa kusimamia mafundisho halisi ya kanisa ya kupiga
marufuku ushoga kama yalivyo kwenye Agano la Kale.
Nguvu kubwa ya vikundi vya kutetea haki za watu
wenye mapenzi ya jinsia moja ni juu ya kauli ya papa Francis aliyoitoa mwishoni
mwa mwaka wa jana alipokuwa kwenye kambi ya vijana wa kanisa hilo huko Rio de
Jeneiro alitoa kauli kuwa kama mtu anamtafuta Mungu na ana nia njema, yeye ni
nani wa kuhoji?
Msimamo huo mpya wa Kanisa Katoliki, huenda ukapata
upinzani mkali kutoka kwa waumini wa kanisa hilo barani Afrika, ambako mapenzi
hayo yamechukuliwa kiasili kama laana na matendo ambayo hata wanyama hawawezi
kuyafanya.
Mara ya kwanza zilipojitokeza dalili za kuruhusiwa kwa
mapenzi hayo na kanisa, viongozi wote wa kanisa hilo barani Afrika walieleza
wazi upinzani wao.
Hata wakati Rais Barack Obama alipozungumzia haki za
kuwaruhusu watu kufanya mapenzi ya kishoga, alipingwa na bara lote la Afrika
likiwemo Kanisa Katoliki la nchini Kenya ambapo Kadinali John Njue alisema hilo
ni jambo ambalo halitakubalika.
Hata hivyo, katika hali ya kutaanisha, kanisa hilo
limesema halitafungisha ndoa za mashoga. Limesema kinachotakiwa ni kutowakana
waumini wao wanaojishughulisha na ushoga kuwahusisha kundini.
Baadhi ya waumini wake wenye msimamo mkali wanaona
kauli hiyo kama iliyo sawa nakuruhusu uzinzi katika kanisa hilo, ambalo hata
wale walioolewa na watu wasio waumini wa kanisa hilo wamekuwa wakichukuliwa
kama wazinifu kiasi cha kutoshiriki ulaji wa mkate wa bwana.
Taarifa zaidi za mkutano huo zinasema, Maaskofu hao
hawajesema kuwa wanaounga mkono ndoa za jinsia moja, lakini Mashirika
yanayotetea haki za mashoga na wasagaji wanasema hatua ya kutambuliwa na Kanisa
Katoliki ni ya kutia moyo.
.jpg)
0 comments:
Post a Comment