KIBANO! Kuonesha wapo ‘serious’ na mavazi, polisi walimtaiti staa wa Bongo Fleva, Rashid Makwiro ‘Chid Benz’ na kumtaka akavae vizuri kisha arejee mahakamani. Tukio hilo lilitokea juzi, Jumanne katika Makahama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar, wakati staa huyo alipokuwa amefikishwa kusomewa mashtaka yake ya kukutwa na madawa ya kulevya. Akiwa katika viunga hivyo vya mahakama, Chid Benz alionekana akiwa ametinga jinzi ambayo ililegezwa mkanda na alipoingia ndani ya chumba cha mahakama, mlegezo uliongezeka zaidi hadi kufikia chini ya makalio kitendo ambacho polisi walishindwa kukivumilia. Kuonesha kwamba hawakufurahishwa na kitendo hicho, maafande waliokuwa wakimsindikiza Chid mahakamani hapo, walimtaiti kwa kumshika kiunoni na kumtoa nje kwenda kumpandisha suruali hiyo kisha kumrudisha akiwa amevaa vizuri.SOMA ZAIDI>>>
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment