Sunday, October 5, 2014


Bwana mmoja nchini Ufaransa amemuoa mke wa zamani wa baba yake (mama yake wa kambo) baada ya kushinda kesi iliyodumu kwa miezi kadhaa.
Harusi ya Eric Holder, 45, na aliyekuwa mama yake wa kambo Elisabeth Lorentz, 48, ilifanyika katika kijiji cha Dabo, karibu na mji wa Metz.

Imeripotiwa kuwa mume wa zamani wa bi harusi, ambaye ni baba wa Bwana Holder, alikuwa miongoni mwa wageni waalikwa.

Sheria za Ufaransa zinapiga marufuku ndoa kati ya watoto wa kambo na wazazi wa kambo, lakini mahakama ilitoa uamuzi wa ndoa hiyo kufanyika.
Ofisi ya mwendesha mashtaka ilipinga uamuzi huo wa mahakama katika eneo la Lorraine, lakini ikaamua kutokata rufaa.SOMA ZAIDI>>

0 comments:

Post a Comment