Wednesday, October 1, 2014

Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Marck Costantine (24), mkazi wa mtaa wa Kitangiri jijini Mwanza amenaswa ‘live’ gesti akiwa na mke wa kigogo mmoja (jina kapuni), aitwaye Mwanaidi wakijiandaa kuvunja amri ya sita.

Baada ya fumanizi kati ya Serengeti boy aliyefahamika kwa jina la Marck Costantine na mke wa kogogo. Tukio hilo lilijiri Septemba 18, mwaka huu kwenye gesti moja maarufu iliyoko mitaa ya Kitangiri baada ya kigogo huyo kupewa ‘ubuyu’ kwamba anaibiwa mali yake ndipo akaandaa mtego na kufanikiwa kumnasa kijana huyo alipokutwa kwenye chumba namba 4 cha gesti hiyo akijiandaa kuserebuka.
“Kigogo alipopewa mchoro huo na wambea, siku ya tukio alimshtua Mwenyekiti wa Mtaa wa Kitangiri, Maginga Patroba, wakatia timu katika gesti hiyo, wakawakuta wachepukaji hao wakiwa kitandani huku Marck akiwa tayari ameshachojoa nguo, Mwanaidi akiwa bado,” kilisema chanzo chetu na kuongeza:
Akisainishwa kulipishwa faini. “Kigogo aliamuru wahudumu wagonge mlango ili wahusika wasishtuke, walipofungua ndipo mwenyekiti sabamba na kigogo huyo wakazama ndani.”

0 comments:

Post a Comment