
Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond’ akwa ameshika gauni la mpenzi wake.
Imebumburuka kwamba staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond’ kumbe anateseka na penzi la mwandani wake, Beautiful Onyinye Wema Isaac Sepetu, Amani lina mkanda kamili.
Kwa muda mrefu kumekuwa na madai kuwa, Diamond amekuwa akiumia na kuvumilia anapoitwa majina mabaya huku akisemekana hamuwezi Wema hivyo awaachie mapedeshee wenye ‘kisu’ kirefu.
“Hivi unajua kwa nini Diamond alimpa Wema zawadi ya Nissan Murano (gari)? Alijua asipofanya hivyo kuna mtu atafanya na kweli ndivyo ilivyotokea kwa lile Gari BMW.“Nawahakikishieni kwa Chibu au Dangote (Diamond) alichezwa na machale,” kilidai chanzo chetu ambacho ni mtu wa karibu wa wawili hao.
Sasa ndani ya pati ya bethidei ya Diamond kwenye Ukumbi wa Golden Jubilee uliopo Posta jijini Dar mwishoni mwa wiki iliyopita, kidume huyo alinaswa akiwa ameshikilia gauni la Wema kwa muda mrefu ili kuhakikisha haliburuzi chini kwa urefu.
0 comments:
Post a Comment