Tuesday, October 14, 2014

Pia mume wa mtu ni sumu! Kikongwe wa miaka 70 aliyejitambulisha kwa jina la Gwerino Ganga amemtwanga risasi mbili mwanaume aitwaye Thadei Mbungu (40) akimtuhumu kuingilia ndoa yake kwa kuvunja amri ya sita na mama watoto wake. 
Thadei Mbungu enzi wa uhai wake.Tukio hilo la ajabu lilijiri Oktoba 9, mwaka huu mkoani Iringa ambapo mashuhuda wanadai Mbugu, mbali na kukutwa na mke wa mtu siku hiyo, alimjibu mwenye mke majibu yenye kuumiza moyo mbele ya watu waliokuwa wakinywa pombe katika klabu cha pombe za kienyeji.Ilidaiwa kuwa, awali mtuhumiwa huyo wa mauaji alikuwa akimsaka marahemu ambaye alidai amekuwa akiivuruga ndoa yake. 
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi aliyefika eneo la tukio, mtoto wa kambo wa mtuhumiwa alisema chanzo cha mauaji hayo ni mke wa Mbungu kumtuhumu mama yake (mke wa mtuhumiwa) kuwa ana tabia ya kukopa fedha kwa mumewe (marehemu) hali iliyosababisha mama huyo kwenda kumwita baba yake (mtuhumiwa) na kumshitakia maneno hayo. 
Mke wa mtuhumiwa.Baada ya kufikishiwa malalamiko hayo, mzee huyo alifika ndani ya klabu hicho na kuanza kumuuliza marehemu juu ya uhusiano wake na mkewe, ndipo marehemu alipotoa lugha chafu mbele ya watu kwa mwenye mke  kuwa ni maskini, hana uwezo wa kutunza wake zake wawili hivyo anasaidia kulea. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI>>>

0 comments:

Post a Comment