MUNGU wangu! Lile sakata la utekaji na upoteaji wa watoto ambao wengi ni wanafunzi wa shule za msingi katika Jiji la Dar na kudaiwa linafanywa na watu walio kwenye magari aina ya Toyota Noah limeingia katika sura nyingine.
Safari hii, gari moja lilitupiwa mawe na dereva nusura kuuawa kufuatia kufika katika Shule za Msingi za Kombo na Mtakuja zilizopo Vingunguti, Dar kwa lengo la kuzungumza na walimu kuhusu mikopo lakini likahofiwa lilikwenda kuteka watoto.
Tukio hilo lilijiri Ijumaa iliyopita na kusababisha vurugu kubwa kati ya wazazi na walimu hali iliyowafanya maafande wa Kituo cha Polisi Buguruni kuwasili katika eneo la tukio ili kutuliza ghasia na kwanusuru walimu.
Gazeti hili lilifika eneo la tukio muda mfupi na kuwakuta walimu wakiwa chini ya ulinzi wa polisi ili wasishambuliwe na wazazi ambao walivamia shule wakidai kwamba watoto watatu walitekwa na watu wenye Noah jeusi. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI>>>
0 comments:
Post a Comment