Sunday, October 19, 2014

NINAMFAHAMU Blandina Changula maarufu kama Johari, tokea akiwa underground wa maigizo katika kikundi cha Kaole, kabla hajapata jina linalomfanya kuwa mmoja wa wakongwe katika filamu Tanzania.
Wakati ule akichipukia, alikuwa mmoja kati ya chipukizi waliokuwa wanaonyesha wazi kwamba watakuja kuwa waigizaji wazuri. Anapatia sehemu nyingi katika sanaa, lakini utampenda zaidi Johari akiigiza sehemu inayohitaji majonzi, au mtu anayetaka kuhurumiwa. 

Johari anaweza kutoa machozi wakati wowote akitaka. Anaweza kucheka kwa sauti na furaha dakika hii, lakini inayofuata akatoa machozi mengi hadi unashangaa. Napata wasiwasi ninapomuona akitoa machozi katika misiba, hujiuliza kama analia kweli kwa uchungu au ni mbwembwe tu za maigizo ili watu wajue ana uchungu! 

0 comments:

Post a Comment