Saturday, October 11, 2014

Mwanamama Neema Iwena aliyekatwa mapanga na mumuwe, Victor Nzali. Kwa mujibu wa mashuhuda wetu, tukio hilo la kutisha, kusikitisha na la ukatili wa kijinsia lilijiri nyumbani kwa wanandoa hao katika Kijiji cha Mlimba, Ifakara mkoani Morogoro na kusababisha vilio kwa kitendo alichokifanya mwanaume huyo cha unyama wa kupitiliza.
Maumivu ya kufa! Akiwa ananyonyesha kichanga wake, dakika chache mwanamama Neema Iwena hakujua kama angenusurika kufa baada ya kukatwa shingoni, kichwani kisha kufyekwa mguu wa kulia na mumuwe, Victor Nzali, kisa kikidaiwa ni wivu wa kimapenzi.

Mmoja wa majirani wa wanandoa hao aliyeshuhudia tukio hilo ambaye aliomba hifadhi ya jina gazetini alisema kwamba, tukio hilo baya maishani lilitokea hivi karibuni ambapo mwanaume huyo alikuwa akimshutumu mkewe kwamba ana mchepuko nje ya ndoa.Neema Iwena akiwa na mwanaye mchanga katika Hospitali ya Rufaa ya St. Francis, Ifakara.SHUKA NAYO HAPA>>>

0 comments:

Post a Comment