Monday, October 20, 2014

Mchungaji mmoja wa kanila Anglican amejikuta matatani baada ya kubambwa uchi kitandani na mke wa mtu, ambaye ni mmoja wa waumini wake jijini Nairobi, Kenya. 

Mume wa mwanamke huyo akiwa amejawa na hasira, anaonekana akimpa kichapo mkewe; huku mchungaji huyo, mwenye pete ya ndoa mkononi kuashiria kuwa ana mke, akivaa nguo zake taratibu. 

Alipoulizwa kulikoni, mchungaji huyo alitoa kisingizio kuwa mwanamke huyo alimuomba aende hotelini hapo kumfanyia maombi. 

Kuongeza msumari wa moto kwenye kidonda, mchungaji na mume wa mwanamke huyo ni marafiki wa muda mrefu. 

Cha ajabu, mchungaji na mume huyo walionekana wakiondoka eneo la tukio pamoja kuelekea kwenye magari yao

0 comments:

Post a Comment