Monday, October 20, 2014

Staa wa sinema za Kibongo, Aisha Bui akiwaka kwa mmoja wa wahusika wa ofisi za kusambaza filamu za Yuneda, Mbagala.
 Staa wa sinema za Kibongo, Aisha Bui amezua timbwili la kufa mtu katika ofisi za kusambaza filamu za Yuneda zilizopo Mbagala jijini Dar baada ya wasambazi hao kushindwa kumlipa kwa wakati. Mtiti huo ulioshuhudiwa na wanahabari wetu ulijiri wikiendi iliyopita, maeneo hayo ya Mbagala ambapo Aisha aliongozana na shemeji yake katika ofisi hizo na kuibua tafrani kubwa iliyokusanya kadamnasi na kufunga mtaa kwa muda.
Aisha Bui mara baada ya kuvunja kioo cha mlango.
Kwa mujibu wa Aisha, amekuwa akitimba kwenye ofisi hizo mara kwa mara akiomba alipwe chake lakini amekuwa akipigwa kalenda tangu Aprili, mwaka huu. Aisha alilifungukia Ijumaa Wikienda kwamba, kuna siku mkurugenzi wa kampuni hiyo aitwaye Ngeze alimwita ofisini kwake ili kumlipa lakini alipofika alimpa kiasi cha shilingi milioni mbili na nusu, jambo ambalo lilikuwa kinyume na makubaliano.SOMA ZAIDI>>>

0 comments:

Post a Comment