Monday, October 20, 2014

Hivi ni kweli kuwa hip hop ni uhuni?
hatuwezi kupata mawezo ya kujenga na ya kimapinduzi kutoka kwenye hip hop?.
Si mwingine bali ni mama mmoja ambae jina lake haikuwa rahisi kufahamika,alikuwa kwenye basi la Shabib kutoka Dodoma kuja hapa dar.
Tulianza safari kama SAA 11:27 am hivi na safari yetu haikuwa ya kuchosha sana kwani tulisindkizwa na nyimbo za wasanii mbalimbali ndani ya basi letu.Zilichezwa nyimbo za kila aina yaani za dini,r&b,blues,bongoflavours nk.lakini kubwa zaidi na lilonifanya nitandaze uzi huu hapa ni kile nilichokishuhudia ndani ya gari baada ya wimbo wa Dear God wa kala J kuchezwa,na kabla haujaisha nikamuona mama mmoja akiangua kilio wakati mda wote..

Mama aliekuwa mda wote akilalama akidai kuwa hapendi anaposhuhudia nyimbo ambazo hazina hata tone la maadili zikichezwa mda wote kwenye gari.
Alienda mbali zaidi kwa kusema mbali na kutokuwa na maadili hazifundishi kitu chochote zaidi ya umalaya.aliongea maneno haya akitoa ushahidi kwa kuonesha kwenye skrini(wakati huo kulikuwa kunachezwa wimbo wa mfa maji wa Say nag).
Alikuwa amekaa kiti kimoja na mzee mmoja ambae bila shaka hakuwa mme wake,
kwani Mbaba huyu alionekana yeye anazukubakai baadhi tu ya nyimbo na kutoka kwa baadhi ya waimbaji(wasanii).
Lakini pia alimwambia nyimbo za kisasa nyingi ni burudani tu , mama yule hakika alionekana anatamani arudishiwe nauli apande gari jingine lakini alikuwa ameshachelewa.
Tulipofika maeneo ya mzani tulianza safari mpya na wimbo wa dogo Aslay,na baada ya mda mfupi ukafuata wa Walewale wa Kala Jelemiah.
Na muda mfupi ukawa unaimba wimbo wa Dear God kila mmoja alimshangaa mama huyu aliekuwa anapaza sauti akilalama kuwa nyimbo za vjana wa leo hata hazifai na kumuomba dereva abadilishe nyimbo au ikiweekana azime kabisa,sasa alikuwa analia akiomba wimbo huo wa kala uchezwe hadi mwisho wa safari yetu.
Tulibaki tunacheka baadala ya kumfta machozi kwani tulijifarji kuwa machozi yale yaliashiria uhondo wa wimbo wa kijana Kala. Mama aliiamini ni WAHUNI.
” kumbe haohao wahuni wanaimba vitu vya maana kabisa,ILA ATAKUWA NI HUYU TU JAMANI NA LAZIMA NIMTAFTE”.alitamka maneno hayo mama huyo alioneka akili yake yote ameiweka kwenye runinga hata tuliposhuka morogoro kupata chochote yeye hakushuka zaidi ya kumuomba Konda asizime redio ili aendelee kula uhondo huku akidondosha machozi ya kushangaa!.
kila abiria alibaki anamuaangalia tu na kumshangaa nikiwemo mim mwenyewe.sjui anawawakilisha wangappi waliokariri ati hip hop au bongofavour ni uhuni!

0 comments:

Post a Comment