Mume wa msanii wa filamu za Kibongo, Ndumbagwe Misayo ‘Thea’, Michael Sangu ‘Mike’ akipozi kimahaba na kiburudisho kipya ndani ya Club East 24, Mikocheni jijini Dar. Kumbukumbu inaonesha, Thea na Mike wamerudiana hivi
karibuni baada ya kumwagana kwa kipindi cha miezi kadhaa kutokana na kupishana kauli ndani ya nyumba. Siku hiyo, Mike na mwanadada huyo ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja, walikuwa wakijiachia ukumbini hapo huku wakipata kinywaji na kushushia na mishikaki ya bata.
Baada ya washakunaku kumshuhudia Mike akitesa na binti huyo, walianza kuizungumzia ndoa yake na Thea na kusikika wakikumbushia ndoa yao jinsi ilivyoyumba kiasi cha wawili hao kutengana kabla ya kurudiana.
Michael Sangu ‘Mike’ akifurahia jambo na binti. “Thea upo? Vibinti kama hivi vya mjini si vya kuviamini vikae na mumeo,” alisikika dada mmoja aliyeomba hifadhi ya jina?
Kufuatia tukio hilo paparazi wetu alifanikiwa kuzungumza na Mike na kumuuliza kuhusu uhusiano wake na mrembo huyo ambapo alisema dogodogo huyo hakuwa akimjua isipokuwa alimshtukia eneo hilo na kumlazimisha amnunulie mishikaki.
“Mimi simjui wala nini nimeshangaa amenivaa ghafla anasema yeye ni shabiki wangu baada ya hapo akaanza kunilazimisha nimnunulie mishikaki na kinywaji,” alisema Mike.
0 comments:
Post a Comment