Profesa Athuman Juma Livigha enzi za uhai wake.
MAUAJI ya aliyewahi kuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Athuman Juma Livigha (63) yaliyotokea nyumbani kwake, Bunju ‘B’, Septemba 30, mwaka huu kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana yameibua mengine ambapo sasa baadhi ya ndugu wamemtaja mwanamke mmoja kuwa huenda anahusika.Wakizungumza na Uwazi siku ya mazishi ya profesa huyo wiki iliyopita, ndugu hao bila kutaka jina la mwanamke huyo walisema kwa asilimia kubwa mwanamke huyo aliyekuwa haelewani na marehemu anatakiwa kufuatiliwa vizuri nyendo zake.
“Huyo mwanamke alikuwa karibu sana na marehemu lakini ghafla akapotea, akawa haonekani na tukasikia yupo tu hapa Dar. Kinachotushangaza hata katika msiba wa profesa hajafika.
“Ni kwa nini kipindi hiki awe muoga wa kuja wakati anafahamika na sisi wanafamilia tunamjua?” alihoji mmoja wa wana ndugu hao ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake.SOMA ZAIDI>>>>

0 comments:
Post a Comment