Mwenyekiti wa BAWACHA ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Kawe kupitia CHADEMA Halima Mdee akiwa katika maandamano akiwaongoza wanawake wenzake kuelekea Ikulu kumpelekea ujumbe Rais Jakaya Kikwete kwamba hasikubali kuweka saini Rasimu mpya iliyopitishwa juzi mjini Dodoma, maandamano hayo kabla hayajafika mbali walitawanywa na jeshi la polisi lililotumia maji ya kuwasha pamoja na kupigwa kwa waandamanaji na kumshika mwenyekiti huyo Halima Mdee pamoja na wafuasi wake na kupelekwa polisi Osterbay.
Polisi wakimpandisha Halima mdee kwenye gari la polisi leo
Mfuasi wa chadema akishikiliwa na polisi na kupelekwa katika gari la polisi

Halima Mdee akiwa ndani ya gari la polisi pamoja na wafuasi wa chadema wakipelekwa katika kituo cha polisi cha Osterbay.

Halima mdee akizozana na polisi mara baada ya kuingizwa kwenye gari
0 comments:
Post a Comment