Friday, October 3, 2014

Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta jana alimchimba mkwara mkewe Margareth Sitta kuwa angepata tabu sana kama angekosea kupiga kura. 
 
Mbali na Uenyekiti wa Bunge la Katiba, Sitta ni Mbunge wa Jimbo la Urambo Mashariki na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na mkewe Margareth ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) na Mjumbe wa Bunge la Katiba.
 
Sitta alitoa kauli hiyo wakati Margareth alipokuwa akipiga kura katika Sura ya 11 hadi ya 19 bungeni mjini Dodoma.
 
“Ungekosea hiyo ungepata tabu sana,” alisema Sitta baada ya mkewe kumaliza kupiga kura katika sura hizo kwa kuzikubali. Hatua hiyo iliwafanya wajumbe wa Bunge hilo kuangua vicheko.

0 comments:

Post a Comment