“Pole
kaka yangu Chidi Benz,Naumia kuona tatizo uliokuwa nalo bado
haujalitaftia jibu unalijua la kutatua tatizo lako,Mimi ni dada yako na
tumeshafanya kazi Pamoja,Tatizo ulilonalo na Mimi nilishakuwa nalo na
niliweza kulitatua sababu nilijitambua na kutafuta suluhu,nimejaribu
kila njia kukushauri badala yake ukaja na rungu la kimasai na
kunitandika nalo nyumbani kwangu!nadhani janga hili lililokukuta
litakuwa Kama jibu kwako kwamba unakoenda si salama kabisa kaka yangu ni
bora ubadilishe njia ili uweze kuungana nasi kwenye tiba ya Methadone
kwani ndio Kiboko ya madawa ya kulevya!!!!Kama Mimi mwanamke nimeweza
najua Hata wewe utaweza!!!!Tanzania bila madawa ya kulevya Inawezekana
!!Watanzania tusimyanyapae Msanii wetu kwani Uteja ni ugonjwa Kama
ugonjwa mwingine na Unazuilika na Kutibika,Ana kipaji na Ana uwezo wa
kurudi tena kwenye Sanaa,Tumuombee mema………Tanzania Stand Up n Wish Him
Luck…………With Love,Ray C Foundation.”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment