Friday, October 31, 2014

Staa mkali wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja.
MASIKINI! Staa mkali wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja hivi karibuni amejikuta akiwa katika wakati mgumu na wa hatari kufuatia watu wasiojulikana kuvamia nyumbani kwake na kutoa onyo kwamba wanampa siku tano tu za kuishi, Amani lina mkasa kamili.Ishu hiyo ya kushtusha ilitokea usiku wa saa nane ya kuamkia juzi, Jumanne nyumbani kwa staa huyo, Sinza Mori jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, watu hao wapatao watatu walitinga nyumbani hapo usiku huo mnene huku wakiwa ndani ya gari aina ya Toyota Rav 4 milango mitano rangi ya bluu ya kuiva na kumkuta mlinzi getini ambaye yupo kwa ajili ya kulinda usalama wa msanii huyo mwenye maadui kila kukicha.“Walikuwa watano, walikuwa kwenye Rav 4 milango mitano, rangi ya blue ya kuiva. Wakamkuta mlinzi, walimuuliza kama Kajala yupo, mlinzi aliwadanganya kwamba hayupo.” 

0 comments:

Post a Comment