KWAKO Miss Tanzania usiyechuja tangu mwaka 2006 hadi leo? Hongera kwa ‘ku-maintain’ ustaa wako tangu miaka hiyo hadi leo.
Ni matumaini yangu u-mzima wa afya. Ukitaka kujua afya yangu, namshukuru Mungu niko poa, naendelea kulisogeza gurudumu la maendeleo kupitia kalamu yangu.Madhumuni ya kukuandikia barua hii si tu kukujulia hali, bali pia kukukumbusha juu ya maisha yako ya kistaa. Eee, we ni staa kwelikweli nani asiyekujua!
Kwa kipindi cha hivi karibuni nimekuwa nikifuatilia juu ya mbwembwe zako na jeuri ya fedha. Ulianzia kwenye Bendi ya Skylight ukafanya kufuru, baadaye mtoto wa kike ukasababisha tena kwa Yamoto Band, kijana Aslay atakuwa kakushukuru kweli kwa mvua ya fedha uliyomwagia.
Yawezekana upo katika ‘kaligi’ ka upinzani na aliyekuwa shosti wako, Kajala Masanja ambaye naye alionesha mbwembwe za namna hiyo hivi karibuni lakini pointi ya msingi hapo ya kujiuliza, zipo nyingi kiasi cha kuzimwaga?
Kila mtu anatambua kwamba fedha zinazotoka bila kuingia mwisho wake ni nini? Zitaisha. SOMA ZAIDI>>>
0 comments:
Post a Comment