Wakati siku za kuelekea tamasha la mwisho la Serengeti Fiesta 2014 zikihesabika, hakuna kinachowapa raha mashabiki wa tamasha hilo nchini zaidi ya kujiandaa na ujio wa mwanamuziki nyota Duniani katika miondoko ya hip hop.
Ama kwa hakika, si mwingine bali ni T.I aliyejipanga kuwashika vilivyo katika jukwaa wakati wa shoo ya tamasha la Serengeti Fiesta 2014 litakalofanyika katika viwanja vya leaders jijini Dar es Salaam hapo Oktoba 18, mwaka huu.
T.I ambye jina lake kamili ni Clifford Joseph Harris, Jr alizaliwa Septemba 15, 1980. T.I ni rapa wa kimarekani, mtengeneza muziki, msanii na mjasiriamali toka Bankhead, Atlanta, Georgia. T.I alianza nyanja zake za kimuziki sambamba na marafiki zake ambao pia ni marapa toka kundi la hip hop la Pimp Squad Click (P$C). Ni mwanzilishi na mtendaji mkuu wa Grand Hustle Records ambayo aliianzisha mwaka 2003. Mwaka 2009, Billboard ilimthaminisha rapa huyo kama msanii bora wa 27 katika kipindi hiki cha miaka ya 2000.
T.I ameshatoa album nane (I’m Serious, Trap Muzik, Urban Legend, King, T.I. vs. T.I.P., Paper Trail,No Mercy na Trouble Man: Heavy Is the Head), zikiwemo saba alizotoa hivi karibuni ambazo zimefanya vizuri sana katika soko la muziki.
Alishinda tuzo tatu za Grammy kupitia fani yake ya muziki. Pia alishatoa nyimbo kadhaa bora kama“Bring Em Out“, “What You Know“, “Big Shit Poppin’ (Do It)“, “Swagga Like Us“ (alimshirikishaKanye West, Jay-Z and Lil Wayne), “Dead and Gone” (alimshirikisha Justin Timberlake), “Ball” (aliyomshirikisha Lil Wayne) na “No Mediocre“ (aliyomshirikisha Iggy Azalea).
T.I alianza kutambulika rasmi katika Nyanja za kimuziki mwaka 2003, baada ya kushirikishwa na rafikiye rapa toka Atlanta Bone Crusher’s single “Never Scared”. Alipata umaarufu zaidi baada ya kutoa wimbo mwingine wa Trap Muzik (2003). Mwaka 2004, T.I alijitokeza katika kumi bora ya Destiny’s Child na wimbo wa “Soldier”, pamoja na Lil Wayne. Albamu ya sita ya T.I, ijulikanayo kama Paper Trail aliitoa mwaka 2008, na kuwa moja ya album bora kabisa kwa sasa, ambayo katika wiki yake ya kwanza ya mauzo iliuza jumla ya kopi 568,000 nchini marekani na kumfanya T.I kuwa mwanamuziki aliyefanya vizuri zaidi kwa mauzo ya album nchini humo.
Albam hiyo inajumuisha nyimbo bora tatu za kimataifa kama “Whatever You Like“, “Live Your Life“(featuring Rihanna) na “Dead and Gone”. Mwaka 2014 amepanga kutoa album yake ya tisa ijulikanayo kama Paperwork na Hustle Gang zilizoandaliwa na studio ya Grand Hustle.
T.I ameshatoa albamu yake ya saba ijulikanayo kama No Mercy mwaka 2010 na pia alifanya vyema katika fani yake ya maigizo katika filamu ya ATL, Takers na Identity Thief zote zikifanya vyema kimauzo. Alichapisha pia vitabu vyake vitatu vya hadithi vijulikanavyo kwa jina la Power & Beauty(2011) na Trouble & Triumph (2012). T.I pia anawika kwasasa katika television nyingi za marekani mfululizo wa kazi zake kama T.I.’s Road to Redemption na T.I. & Tiny: the Family Hustle.
0 comments:
Post a Comment