Saturday, October 4, 2014

Utapeli mzito umeshamiri Bongo ambapo imebainika kuna taasisi iliyojipachika jina la Tanzania Loan Society inayojieleza kuwa inafadhiliwa na Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano wa Serikali ya Marekani huku ikiwarubuni watu kuwa inatoa mikopo bila riba.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Jakaya Mrisho Kikwete.Ipo kimtandao zaidi
Taasisi hiyo iliyoanzishwa muda mrefu ikapotea, sasa imeibuka upya na inawaliza wengi ambapo inaendesha shughuli zake kimtandao na wahusika hutumia utundu kuingilia mawasiliano katika akaunti za watu katika facebook na kuweka ushuhuda kuwa wamiliki wamefanikiwa kupata mkopo bila riba tena kwa masharti rahisi. Mtandao umegundulikaje?
Mmoja wa wasomaji wa gazeti hili aliyefahamika kwa jina la Lulu, hivi karibuni alileta malalamiko yake akieleza jinsi wahusika wa utapeli huo walivyoingilia mawasiliano yake ya Facebook, wakamlisha maneno kuwa aliomba mkopo wa shilingi milioni 3 baada ya kutoa shilingi 95,000 kwa ajili ya uanachama na akapewa fasta. 

Kwenye ukurasa wa Facebook wa Lulu, kulikuwa na maelezo ya kupika kuwa, Tanzania Loan Society ni taasisi iliyo chini ya Rais Jakaya Kikwete kwa msaada wa Rais wa Marekani Barack Obama huku watendaji wakuu wakiwa ni Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda na Mbunge wa Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete. 

Ikadaiwa eti muweka hazina wa taasisi hiyo ni Zainabu Kikwete huku namba zake za simu zikitajwa kuwa ni 0767 602 518 na 0713 009 819, lengo la mpango huo likiwa ni kuhakikisha Watanzania wanaondokana na umaskini kwa kupewa mikopo kwa masharti nafuu. 

0 comments:

Post a Comment