Tuesday, October 7, 2014


WAJUKUU wa marehemu Sabina Ngalu (77) wameibua kutuko makaburini kufuatia kuzama ndani ya kaburi la marehemu huyo na kugoma kutoka wakidai kwamba mpaka walipwe shilingi laki moja (100,000), Uwazi lina mkanda mzima.

Wajukuu wa bibi huyo wakiwa kaburini. Tukio hilo la aina yake lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita katika Kitongoji cha Nyamwanza Kata ya Sima wilayani Sengerema mkoani Mwanza muda mfupi baada ya mwili wa marehemu kuwasili eneo la mazishi kwenye shamba lake ukitokea Kanisa la Roman Katoliki Parokia ya Yesu Kristo Mfalme la mjini Sengerema. 
Sababu za wajukuu hao kung’ang’ania ndani ya kaburi hilo walitaka wapewe ng’ombe mmoja au pesa hizo taslimu kwa mjibu wa mila na desturi za kabila la Kisukuma jambo ambalo lilipingwa na baadhi ya wanandugu waliodai mila hizo zilipitwa na wakati. 
Kufuatia wajukuu hao kuendelea kugomea ndani ya kaburi, kaka wa marehemu, Enosi Ngalu alikwenda kukata fimbo na kuwashukia kisha kuwacharaza viboko wote huku nao wakisisitiza hawatoki mpamka ‘kieleweke’.

0 comments:

Post a Comment