CREDITS; RAMADHANI CHILEMBA
Wananchi wenye hasira kali wamewaua na kuwachoma moto watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni majambazi.
Tukio
hilo limetokea leo tarehe 08/10/2014 saa 4:00 Asubuhi katika kitongoji
cha NAMANDUNGUTUNGU, maarufu kama MANZESE, kijiji cha SOMANGA, Wilaya ya
kilwa Mkoa wa Lindi.
Watu
hao wameuawa ikiwa ni siku moja tu tangu Alipotekwa, kupigwa na kuuawa
Mwendesha pikipiki mmoja, maarufu kama bodaboda aliyeulikana kwa Jina la
SELEMANI POMBE Mkazi wa Kijiji cha Somanga siku ya Tarehe 06/10/2014
saa mbilin usiku.
Mwendsha bodaboda huyo alipigwa na kuuawa kisha kunyang`anywa pikpiki yake aina ya SUNLG yenye Namba za usajili T678 CYB.
Tukio hilo limetokea katika eneo la Mitondo kijiji cha Somanga simu.
Mwendesha
pikipiki huyo alitekwa na kuuawa alipokuwa anampeleka abiria wake
katika kitongoji cha Mitondo na inasemekana abiria huyo alikwenda
kukagua mkaa wake. Abiria huyo alifanikiwa kuwatoroka Majambazi hao
baada ya kufanikiwa kufungua kamba alizokuwa amefungwa mikononi na
miguuni baada ya kumjeruhi vibaya na kumbaka.
Watuhumiwa hao wa ujambazi wanasadikiwa kuwa ndio wanaofanya uhalifu
katika maeneo ya NYAMWAGE-MUHORO-MARENDEGO-SOMANGA, maarufu kama Eneo la
Vumbi. Wanateka magari,na kujeruhi watu, kulawiti na kuwanyang`anya
fedha na mali zingine kama simu, computer n.k
Mwandishi
wa Habari hizi amefanikiwa kupata jina la mmoja aliyeuawa kuwa ni
RAMADHANI MAKUNGWA mwenye umri wa miaka 30, mkazi wa kijiji cha Somanga,
na mwingine hatujuweza kupata jina lake lakini kwa taarifa kutoka kwa
baadhi ya raia zinasema mtu huyo ni Mwenyeji wa Lindi lakini yupo katika
eneo hilo kwa Muda mrefu kidogo.
Kuuawa
kwa watu hao kumetokana Na msako mkali ulioendeshwa na wananchi baada
ya kukithiri kwa matukio ya ujambazi katika maeneo ya kilwa kama
Nangurukuru, Miteja,Kipatimu,Njinjo,na somanga.
Kwani
Mnamo tarehe 03/10/2014 majira ya saa 4:30 usiku, gari zaidi ya kumi
zilitekwa na Abiria, madereva na mautingo kuporwa mali na fedha pamoja
na baadhi yao kubakwa na kulawitiwa na wengine kujeruhiwa Vibaya.
Tukio hilo la kusikitisha na kuhuzunisha limetokea katika kijiji cha SNZA-MITEJA.
Baada
ya kuwakamata watu hao kabla ya kuwaua, mmoja alisema wasimuue
ataonesha ni wapi wenzao watatu walipo pamoja na pikipiki lakini
kutokana na hasira za wanachi waliwaua na wengine wamezagaa katika pori
la MIBUYU SABA raia aliyetoa taarifa za kuonekana kwa watu hao na
kufanikiwa kuwakamata hao wawili aliwaona watu hao.
Hivyo
Mpaka wakati huu msako unaendelea, Wananchi wengi wamezagaa na
kuzingira pori lote la MIBUYU SABA kuwasaka hao watatu waliosalia pamoja
na pikipiki zilizoporwa.
MOTO UUONAO HAPO KWENYE PICHA HAPO CHINI NI HAO MAJAMBAZI WAKICHOMWA BAADA YA KUUAWA
0 comments:
Post a Comment