Thursday, November 27, 2014


Binti Ester Sako (26)akiwa nyumbani kwao katika kijiji cha Msagara Wilayani Kishapu mkoani Shinyanga 


Ester Sako


Ester Sako ni msichana mwenye umri wa miaka 26 alizaliwa

akiwa na ulemavu wa ngozi Albino lakini mnamo mwaka 2011,alipata kipele sehemu za usoni karibu na pua.



Baada ya kupata kipele hicho alikitumbua ndipo majimaji

 yalianza kutoka na kusababisha kupata uvimbe ambao kila siku unamsababishia vidonda usoni.



Ester Sako anaishi kwenye kijiji cha Msagara Wilayani
Kishapu Mkoani Shinyanga ambapo kufuatia vidonda hivyo
vilivyoenea usoni kwake anaomba wasamaria wema wajitokeze kumsaidia kwani wakati mwingine vipele hivyo vinatoa wadudu wadogo wadogo weupe.

0 comments:

Post a Comment