LEMUTUZ

Saturday, November 1, 2014

ASKARI POLISI WA KIKE MWANZA AMKATA VIDOLE VINNE MFANYAKAZI WAKE KWA PANGA AKIMTUHUMU KWA KUMWIBIA DEKI YA VIDEO.

Posted by Williammalecela.com on Saturday, November 01, 2014
JESHI la Polisi mkoani Mwanza linamshikilia askari wake WP Fatuma wa Kituo cha Polisi Igogo wilayani Nyamagana kwa kosa la kumjeruhi mtumishi wake wa ndani kwa mkumkata vidole vyake vinne vya mkono wa kulia kwa panga, akimtuhumu kumwibia Deki ya Video nyumbani kwake. 
Tukio hilo la kujeruhiwa kijana Steven Magessa (18), lilitokea Oktoba 20 mwaka huu katika kijiji cha Magange Mugumu wilayani Serengeti mkoani Mara nyumbani kwao kijana huyo aliyekuwa amekimbilia huko baada ya kudaiwa kumwibia mwajili wake nyumbani eneo la Igogo.
AKIONYESHA NAMNA ALIVYOJERUHIWA NA MAMA HUYO
Akizungumza na waandishi wa habari kijana huyo alieleza kuwa kufanya kazi kwa askari huyo kulikuja mara baada ya askari huyo kumfuata kijijini na kumuomba ridhaa ya wazazi wa kijana huyo kuambatana naye jijini Mwanza ili kumsaidia kazi za nyumbani ambapo walikubaliana malipo ya kiasi cha Sh 50,000/= kila mwezi jambo ambalo askari huyo alilikiuka na kushindwa kulitekeleza kwa muda wa miezi sita bila kumlipa mshahara.PICH ZAIDI>>>
Email ThisBlogThis!Share to XShare to Facebook
Newer Post Older Post Home

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to: Post Comments (Atom)

TOTAL PAGEVIEWS

Popular Posts

  • LIVE: RAIS MAGUFULI ANAKABIDHIWA RIPOTI YA UCHUNGUZI WA MADINI
  • BREAKING NEWZ: BASI LA NGANGA LATUMBUKIA MTARONI KULIKWEPA LORI
  • THE UDAKUZ: WEMA SEPETU Vs WOLPER!!
  • IRAN NA MAREKANI WAZIDI KUIMARISHA UHUSIANO
  • PICHA YA KWANZA YA KANISA LA ASKOFU MTATA GWAJIMA BAADA YA KUKUMBWA NA BOMOA BOMOA YA SERIKALI JANA LIVE.
Copyright © LEMUTUZ

Developed by MKCT